Wednesday, May 11, 2011

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOHAMA!

                                              Profesa JOHN NKOMA (Kushoto)

Vyombo vya Habari nchini Vimetakiwa kuhamasisha matumizi ya Teknolojia za Mawasiliano ya Kisasa ili iweze kutumika katika sekta mbalimbali za Ki-Jamii kwa lengo kuharakisha maendeleo katika Nyanja tofauti hapa nchini.

Akifungua Warsha ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Jijini DSM, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Dakta VUAI LILA amesema wanahabari wanatakiwa kujiwekea mikakati ya kuandaa makala za vipindi vinavyolenga kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu Ubora na uzuri wa matumizi ya Teknohama.
Aidha kwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa (TCRA) Profesa JOHN NKOMA amesema kwa kutumia Sera na Sheria zilizopo mamlaka hiyo itahakakikisha kwamba wananchi walio pembezoni wanafikiwa na huduma za Msingi za mawasiliano ili kufikia malengo ya Serikali.

No comments:

Post a Comment