Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, AGGREY MWANRI amewataka watendaji wa Manispaa nchini kujiandaa na ujio wake katika maeneo yao ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la Rais JAKAYA KIKWETE linalowataka Mawaziri kuacha kufanyia kazi maofisini.
Akizungumza wakati wa ufungaji Mkutano wa 27 wa watendaji wa TAMISEMI (ALAT ) ,Naibu Waziri MWANRI amesema katika kila Halmashauri atakayoenda ataomba ripoti ya ukaguzi wa ndani ili kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya kimaendeleo hususani katika maeneo ya vijijini.
Aidha amewaagiza watendaji wote wa Halmashauri ikiwemo madiwani kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo amebainisha kuwa wana uwezo wa kuongeza kasi ya kuleta mabadiliko kutokana na nafasi waliyonayo.
No comments:
Post a Comment