Tuesday, July 17, 2012

BHAKRESA AWA MTEJA WA KWANZA KUNUNUA GARI MPYA AINA YA 'VOLKS WAGON AMAROK' NCHINI


Haya ndio Magari Mawili aina ya 'VOLKS WAGON AMAROK' yaliyonunuliwa na Mfanyabiashara maarufu nchini Said Bhakresa.

Pichani Juu na Chini ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD inayouza magari hayo Bw. Julius Guni(kushoto) akimkabidhi Funguo pamoja na Manual Book za magari hayo mwakilishi wa mzee Bhakresa Bw. Omar Said kutoka Bhakresa Food Products.Bw. Omar Said katika pozi baada ya kukabidhiwa rasmi magari hayo.Bw. Omar Said akichomeka funguo kuwasha moja ya magari hayo.Wow.....Kweli ni 'VOLKS WAGON AMAROK'.

Volks Wagon 'Amarok' za Mzee Bhakresa.

Mwakilishi kutoka kampuni ya Bhakresa Food Products Bw. Omar Said akikagua Injini ya moja wapo ya gari hizo sambamba na Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni.
Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Alfred Minja akiwajibika ofisini kwake kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na wateja wanapata taarifa za kutosha kuhusiana na kampuni hiyo pamoja na magari wanayouza.
Kanpuni hiyo imeanza kazi rasmi tarehe 1 Julai mwaka huu chini ya Mkurugenzi huyo mpya na tayari leo tarehe 11 Julai wamefanikiwa kuuza magari mawili aina ya 'VOLKS WAGON AMAROK'.
Pichani Juu na Chini ni Fundi wa Kampuni ya Alliance Auto (T) LTD Bw. Dennis Dismas akifanya Services ya Magari ya Wateja wa Kampuni hiyo kwa Teknolojia ya kisasa inayotumia Kompyuta.

Mzigo wa kutosha wa magari aina ya 'VOLKS WAGON AMAROK' katika yadi ya kampuni ya Alliance Autos (T) LTD iliyopo barabara ya Pugu/Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment