Thursday, April 12, 2012

BADEF Charity Walk

                                                      Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

12/04/2012

Barwany Albinism Development Trust Fund (BADEF) Kupitia Kampeni ya Nifahamu Itafanya matembezi ya Hisani Ya Kuchangisha Na Kukuza Ustawi wa Walemavu wa Ngozi Nchini

• Yazindua matembezi ya hisani yatakayofanyika 14/04/2012 kuchangisha fedha ili kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini

• Mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Dkt. Hadji Hussein Mponda (MB) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.

Dar es Salaam Tanzania, Aprili 12, 2012 – Taasisi isiyo ya kiserikali Barwany Albinism Development Trust Fund (BADEF), kupitia kampeni ya Nifahamu iliyozinduliwa Disemba mwaka jana yazidi kuimarisha ustawi wa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini. Jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inatengwa na kunyanyasika sana. BADEF, kwa kutambua hilo imeandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kukusanya kiasi cha fedha cha Tsh. Milioni 500 kwa ajili ya kuchangia ili kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

 Mh. Salum Khalfan Barwany ambaye ni mwenyekiti na mwanzilishi wa BADEF awaomba Watanzania kushiriki na kuunga mkono kampeni hii kwenye matembezi ya hisani yatakayofanyika tarehe 14/04/2012 saa kumi na mbili asubuhi. Matembezi haya yataanzia kwenye viwanja vya Leaders Club kinondoni mpaka viwanja vya Mnazi Mmoja . BADEF itazitumia fedha hizi kuwasaidiwa walemavu wa ngozi kupitia njia zifuatazo:

a).Kufanya tafiti mbalimbali juu ya hali ya watu wenye ulemavu wa ngozi kv. Kielimu, kiafya na kijamii;

b).Kutoa elimu ya ulemavu wa ngozi;

c).Kuhamasisha ujumuishwaji kwenye sekta mbalimbali nchini na;

d).Kutoa vifaa vya kukinga

“Nikiwa miongoni mwa walemavu wa ngozi, nimeanzisha shirika lisilo la kiserekali (BADEF) linalohusika na kuleta ustawi kwenye maisha ya walemavu wa ngozi nchini.Mh. Barwany alisema. “kupitia Kampeni hii ya Nifahamu tunatoa ujumbe ufuatao:



a).Nilinde – Nina haki ya kuishi kama binadamu mwingine yeyote, pia nahitaji hifadhi ya maisha yangu.

b).Nijali – Ninastahili heshima, kuthaminiwa na kupewa huduma na mahitaji maalumu

c).Nielimishe – Niwezeshe kujitambua, na kujilinda na jamii initambue na kunilinda

d).Naweza – Ninastahili kupewa fursa kama binadamu mwingine yeyote

e).Nipende – Mimi ni mwanadamu kama mwingine yeyote na ninastahili furaha, mapenzi na huruma.

Nawaomba watanzania wenzangu kuungana na mimi kwa kushiriki kwenye kampeni ya Nifahamu. Lengo kuu la kampeni hii ni kuelimisha jamii kuondokana na mtazamo hasi kwa walemavu wa ngozi nchini ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi sasa.

Mtazamo huu umechangia kuleta maafa mbalimbali kwa walemavu wa ngozi, kwa mfano: mauaji ya kikatili, kukatwa kwa viungo vyao na hivyo kuwaongezea ulemavu zaidi, kutengwa na kutohusishwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni”. Aliongeza

Alizidi kusema,“Walemavu wa ngozi wanachangamoto nyingi sana katika jamii. Ukiachana na mtazamo hasi, wanakumbwa na majanga mengi yafuatayo: hatari ya ugonjwa wa saratani ya ngozi, imani potofu, uoni hafifu na jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya ulemavu wa ngozi.

“Vilevile unaweza kuchangia kupitia: Mpesa Namba; 0769696999, Airtel Money Namba; 0688858535, Tigo PesaNamba; 0655029595 au kwenye akaunti ya BADEF (CRDB Bank, Lumumba Branch Akaunti Na. 0150278228900).” Kufanikisha kampeni hii tunahitaji ushirikiano wa hali na mali kutoka kwa kila Mtanzania. Tunatumaini utaguswa na kujali kuungana nasi.”

Kwa maelezo zaidi kuhusu kampeni hii na matembezi ya hisani, ungana na wasiliana nasi kwenye mtandao kupitia:

Facebook: www.facebook.com/Nifahamu
Twitter: www.twitter.com@Nifahamu,
Barua pepe: skbarwany@gmail.com,
Simu: 0713 690 637

Kwa mawasiliano:
Simu: 068624027

No comments:

Post a Comment