Thursday, February 23, 2012

WACHIMBAJI KOKOTO KUNDUCHI WAAANZA KUYAHAMA MACHIMBO HAYO KUTII AMRI YA SERIKALI!

Baada ya Serikali kutoa siku tano kwa wachimbaji wa kokoto katika machimbo ya Kunduchi, Jijini Dar es Salaam kusitisha zoezi hilo katika machimbo hayo hatimaye wameanza kutii agizo hilo na kuanza kuondoka eneo hilo.



Wakizungumza na kituo hiki wachimbaji hao wamesema, wameamua kuchukua hatua hiyo ili kutekeleza agizo la Serikali lililowataka kuondoka eneo hilo ifikapo Februari 23 mwaka huu huku wakibainisha kuwa wameshaunda umoja wao utakaowasaidia kuwezeshwa na serikali.

No comments:

Post a Comment