Thursday, February 23, 2012

KINYWAJI CHA KIBUKU KUINUA MAISHA YA MKULIMA!

Imeelezwa kwamba licha ya kinywaji cha Kibuku kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa ikiwemo kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi hususani kwa wafanyabiashara ndogondogo, pia kinasaidia upatikanaji wa soko la mazao kwa wakulima nchini.



Akizungumza Jijini Dar es Salaam Meneja Mauzo na Usambazaji wa Darbrew Limited ambao ni wazalishaji wa Kibuku Bw URBAN SHAYO amesema tayari baadhi ya wakulima wamenufaika kwa kupatiwa elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha kupandisha thamani ya mazao yao ikiwemo mahindi na mtama.

No comments:

Post a Comment