SERIKALI imeingia mkataba wa miaka 11 na kampuni ya Swala Oil and Gas utakaohusisha utafutaji wa mafuta na gesi maeneo ya Kilosa, Kilombero mkoani morogoro na Pangani mkoani Tanga ukiwa na lengo la kuhakikisha serikali inafaidika na rasilimali zilizopo nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema serikali inaingia mikataba mbali mbali ya utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi ili kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha mafuta kama nchi zingine za Afrika ifikapo mwaka 2023.
No comments:
Post a Comment