Thursday, February 16, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MRADI WA MTO MKUJU-MADINI YA URANI WA MANTRA TANZANIA!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Usalama Kazini, Nassor Abdallah, kuhusu vifaa vya usalama kazini vinavyotumika na wafanyakazi wa migodini wanapokuwa kazini, wakati Makamu akiwa kazitika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma jana Februari 15, alipotembelea mradi wa Mto Mkuju unaojiandaa na uchimbaji wa madini ya Urani kupitia kampuni yake ya Manta Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mjiologia Mkuu wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Emmanuel Nyamusika kuhusu utafiti wa upatikanaji wa madini ya Urani, wakati Makamu akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma jana Februari 15, alipotembelea mradi wa Mto Mkuju unaojiandaa na uchimbaji wa madini ya Urani kupitia kampuni yake ya Manta Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammeed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa Wazee wa Kijiji cha Likuyu Sekamaganga, baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma jana Februari 15, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment