Monday, November 7, 2011

KUELEKEA MIAKA 50 YA UHURU, SHUHUDIA HALI HALISI YA MAISHA YA WATANZANIA!

Wakati Taifa likielekea kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, bado hali ya wananchi wa Tanzania kiuchumi ni ya kujikongoza na inayosadikika ingawa baadhi yao wamejiingiza kwenye ajira binafsi kama wanavyoonekana akina mama hawa wafanyabaishara za matunda na mbogamboga wanavyoonekana wakiwa kwenye usafiri wa Baiskeli ya matairi matatu maarufu kama Guta.

Mwendesha Guta huyu naye yupo kazini, inawezekana amewapakiza kwa ujira kidogo au sio vibaya kusikia kwamba amewasaidia ili kuwafikisha huko waendako. Ni miaka 50 ya Uhuru na taifa liko kwenye maandalizi ya shamrashamra hizo za kilele kitakachofanyika Desemba 9 mwaka huu. VIVA TANZANIA, VIVA AFRICA! Picha na SAID KHAMIS.

No comments:

Post a Comment