Tuesday, November 8, 2011

MBUNGE WA MEATU SHINYANGA APINGANA NA MKUU WA MKOA ALIYEWATAKA WANAOISHI KWENYE HIFADHI KUHAMA!

Mbunge wa jimbo la Meatu Mkoani Shinyanga Meshack Opulukwa amedai kuwa hakubaliani na kauli ya Mkuu wa Mkoa Nassoro Lufungo ya kuwataka wakazi wanaoishi karibu na hifadhi ya a wanyamapori ya Makao (WMA ) waondoke kwa sababu kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuwanyima haki zao wanazopaswa kupewa.

Mbunge huyo amesema kuwa hapingani na kuwepo kwa mwekezaji huyo katika jimbo lake bali anachopinga ni kuhamishwa kwa wananchi bila kufuata taratibu za nchi zinazotaka haki itendeke wakati wa kumpisha mwekezaji.


Amesema kuwa mkuu wa mkoa hapaswi kuwambia wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo wahame mara moja bali anachotakiwa kukifanya ni kuangalia upya suala zima la kuwahamisha ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za kuwahamisha wananchi hao ikiwa ni pamoja na kupitia upya mikataba iliyopo.

2 comments:

  1. jamani ukweli ubaki kuwa ukweli wanoondoshwa si wanao kaa karibu na WMA bali waliohamia na kuamua kuishi ndani ya pori la akiba.

    Dkt. Opulukwa kusema ukweli ni uungwana

    ReplyDelete
  2. Doctor Mpaka kuitwa doctor naamini atakuwa amesha fanya tafiti za kutosha. USHAURI wa bure Fanyia utafiti swala la WMA Soma sana usichoke soma nyaraka zilizopelekea kuundwa kwa WMA.

    Halafu kwa uelewa wangu kuhusu Mwekezaji yeye amewekeza ktk pori la akiba la Makao ila ameingia mkataba na vijiji vinavyounda WMA kusaidiana kuilinda na kimsingi kama ambavyo vijiji vinavyopakana na WMA yeye pia kitalu chake kinapakana nayo.

    Simple logic nayeye anawajibu kushirikiana na vijiji kuilinda WMA.

    NAUNGA MKONO KUHAMISHWA wewe nakushauri uwe nyutro kuzilinda kura zako aidha ukigangamala mwisho wake aibu.

    ReplyDelete