Sunday, November 20, 2011

SIKU MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ALIPOFUNGUA MDAHALO WA NAFASI YA UMUHIMU WA KATIBA KTK MAISHA YA WATANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku (wa pili kushoto) wakati akiiwasili kwenye Jumba la Makumbusho ya Taifa leo Novemba 17 kwa ajili ya kufungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo Novemba 17, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika maonyesho ya Jumba la Makumbusho ya Taifa kuangalia picha za baadhi ya Mashujaa wa Harakati za ukombozi zilizowekwa katika jumba hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim na (kulia) ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika jumba hilo na kuangalia baadhi ya picha za matukio zilizowekwa katika jumba hilo kama kumbukumbu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati) wakiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA) Willbroad Slaa, nje ya ukumbi, wakati Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo Novemba 17, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment