Tuesday, November 29, 2011

SHIRIKA LA SIKIKA LAIPONGEZA SERIKALI KUCHAPISHA BAJETI YA SERIKALI 2011/2012 KWENYE TOVUTI!

Taasisi ya SIKIKA kwa kushirikiana na mashirika mengine imeipongeza Serikali kwa kitendo cha kuchapisha bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 kwenye tovuti yake , na kusema kwamba hatua hiyo imewawezesha wananchi kufuatilia mjadala wa bajeti na kuishauri Serikali namna ya kutatua kero zinazowakabili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo IRENEI KIRIA amesema licha ya SIKIKA na mashirika mengine kutoa rai kwa Wizara ya Fedha na Uchumi kuchapisha vitabu vya bajeti, Serikali ilikuwa haitoi taarifa juu ya fedha za walipa kodi zinavyotumika katika taasisi mbalimbali za umma.


Kutokana na hilo taasisi ya Sikika imewaomba wananchi kutembelea tovuti ya Wizara ya Fedha kupitia www.mof.go.tz na kutumia fursa hiyo kutafakari kama serikali imeweka kipaumbele katika kutekeleza miradi ya elimu na afya.

No comments:

Post a Comment