Tuesday, November 29, 2011

CCM:KIKAO CHA NEC DODOMA HAKIKUMTUHUMU WALA KUMSAFISHA KIONGOZI YEYOTE

Chama Cha Mapinduzi CCM, kimeeleza kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika hivi karibuni Mjini Dodoma hakikumtuhumu wala kumsafisha kiongozi yeyote ndani ya Chama hicho, bali kilifanya mchakato wa kukasimisha madaraka kutoka Kamati ya Maadili na kuwa Tume kamili.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho, WILLSON MUKAMA, amesema lengo la kukasimisha majukumu ya Kamati ya Maadili ni kuwezesha kutekelezwa kwa maazimio 27 yaliyofikiwa na Halmashauri hiyo, ikiwemo kuchukua hatua dhidi ya viongozi wanaohusishwa na suala la Ufisadi.


Katibu mkuu huyo ameongeza kuwa kutokana na baadhi ya viongozi wanaohusishwa na suala la Ufisadi kutochukua hatua wao wenyewe, CCM kupitia tume iliyokasimu madaraka itawachukulia hatua mara moja baada ya kufanya uchunguzi na kumhoji kila anayetuhumiwa kwa suala hilo.

No comments:

Post a Comment