Tuesday, November 29, 2011

NHC LATOA UFAFANUZI KUHUSIANA NA VURUGU ZA UBUNGO NHC!

Shirika la Nyumba la Taifa NHC limewaondoa hofu wakazi wa kota za Ubungo kwamba halina mpango wa kuvunja nyumba wanazoishi na badala yake wanaendeleza makazi hayo ili yaendane na mahitaji ya watu.

Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki Meneja Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC Bw MUUNGANO SAGUYA amesema fujo zinazotokea katika eneo hilo zinatokana na kikundi cha watu kushinikiza kwamba shirika hilo lina mpango wa kuwahamisha wapangaji wote ili kujenga maghorofa mapya.


Katika hatua nyingine shirika hilo limewatadharisha watu wote wanaozuia kazi za ujenzi kuendelea katika eneo hilo kwamba watafikishwa katika vyombo vya dola ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment