Wednesday, November 2, 2011

EXCLUSIVE: MBWANA SAMATTA AVUNJA REKODI CONGO - AFUNGA MAGOLI 6 KWENYE MECHI MOJA!

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe leo amefanya maajabu makubwa katika historia ya soka la nchini Congo baada ya kufunga magoli 6 kati ya 13 yaliyowekwa kimiani na TP dhidi ya FC Police katika michuano ya ligi ya jimbo la Katanga.

Mbwana Samata amekuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga idadi hiyo ya magoli katika mechi moja hivyo kuweka rekodi ndani ya klabu yake.Magoli mengine katika mechi hiyo iliyoisha kwa TP Mazembe kushinda ugenini kwa mabao 13-1 yalifungwa na Wachezaji, Lusadisu (3 ), Kanteng, Traore ( 2 ) na Mabele.

No comments:

Post a Comment