Wednesday, October 12, 2011

ZAIDI YA BILIONI 100 KUTUMIKA KUJENGA MJI MPYA WA ILIYOKUWA MAGOMENI KOTA!

                 Baadhi ya wakazi wa Magomeni kota wakiomba dua kabla ya moja ya kikao chao.

Zaidi ya shilingi bilioni 100 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mji mpya wa magomeni kwenye eneo la magomeni kota Manispaa ya Kinondoni jijini DSM lenye ukubwa wa ekari 150.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Meya wa Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA amesema ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa ujenzi huo tayari wananchi wanaoishi kwenye nyumba hizo wameanza kulipwa feha za pango la mwaka mzima ambapo kila kaya imepatiwa jumla ya shilingi milioni moja, laki moja na elfu hamsini.


Amesema wananchi hao wanapaswa kuondoka ifikapo Desemba, 30 mwaka huu na kubainisha kuwa anayetaka kubomoa na kuchukua matofali, vigae, madirisha au milango anaruhusiwa kwani kinachotakiwa ni kubaki wazi kwa eneo hilo tayari kwa ujenzi.


Aidha meya huyo amewataka wananchi wa Manispaa ya Kinondoni kuonyesha ushirikiano kwa watu wanaohusika na usafi wa mazingira mitaani na kubainisha kuwa kampuni ya Majembe Oksheni Maty imepewa jukumu la kusimamia usafi barabarani.

No comments:

Post a Comment