Wednesday, October 12, 2011

SERIKALI KUBADILISHA MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WAKE!

Serikali imesema katika kukabiliana na tatizo la Watumishi hewa imeamua kubadilisha na kuboresha zaidi mfumo wa malipo ya mishahara kwa watumishi wake.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma Bi HAWA GHASIA, amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo hilo kwa asilimia 90 kwa kuwaruhusu waajiri wao kushughulikia taarifa za watumishi wao kuliko kutegemea zaidi Utumishi na hazina.


Katika hatua nyingine Wizara hiyo inatarajia kufanya kongamano la kumbukumbu ya miaka kumi na miwili tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS K. NYERERE kwa lengo la kuielimisha na kuikumbusha jamii juu ya mambo muhimu ambayo Baba wa Taifa aliyaamini na kuyafuata huku Raisi Mstaafu wa awamu ya nne, BENJAMIN WILLIAM MKAPA, akitarajiwa kuwa Mwenyekiti wa kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment