Sunday, October 9, 2011

WAJUMBE WA BARAZA LA USALAMA BARABARANI TAIFA WATEMBELEA BAR YA MTUKULA-KAGERA!

                                Hapa ni Kilometa 20 kabla hujafika Mtukula ukitokea Kagera

Na Jonathani Tossi wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera

Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani Taifa wakiwa wafutana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Mohamed Mpinga wafanya ziara katika barabara itokayo mkoani Kagera kwenda katika mpaka wa Watanzania na unganda eneo la mtukula yenye urefu wa kilomita themanini (80) na kuona changangamoto zinazo sababisha ajali za mara kwa mara katika barabara hiyo ya Kagera Mtukula


Akizungumza katika ziara hiyo kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kagera Sp Marisoni Mwakyoma amesema ajali nyingi zinazo tokea katika eneo la Omkajunguti wilaya ya Misenyi zinasababishwa na wafungaji ambao huchunga mifugo kandokando ya barabara pia amesema sababu nyingine ni kutokana na madereva ambao uendesha magari kwa mwendo kasi bila kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani za barabarani .

Pia amesema suala jingine ni kwa madereva ambao wazoea kuendesha magari nchini Uganda kwa mtindo wa kupita kulia na wapokuja nchini hushindwa kubadilika haraka na kusababisha ajali .


Nao wajumbe wa kamati hiyo ya usalama barabarani taifa wametoa mapendekezo yao kwa wakala wa Tanroads kujenga matuta madogomadogo aina ya rasta ilikuzidhibiti ajali zinazopoteza maisha ya wananchi mkoani Kagera na nchini kwa ujumla pia wamependekeza kuwapo kwa alama za barabarani zinazo onesha kuwepo kwa vivuko vya wanyama katika barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment