Sunday, October 16, 2011

KCB TANZANIA KUTUMIA MILIONI 180/- KUADHIMISHA WIKI YA JAMII!

Wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakipanga viroba vya vyakula wakati hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5/- kwa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam.
Watoto wanaoishi katika kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam wakifurahi baada ya kukabidhiwa msaada wa Vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya milioni 4.5/- kutoka kwa Benki ya KCB Tanzania hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa akizungumza na Walezi na watoto wanaoishi katika Mazingira magumu wa kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya milioni 4.5/- kutoka kwa benki hiyo hivi karibuni.Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano Bi Christine Manyenye na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Moezz Mir.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa akikabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5/- kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Friends of Don Bosco Theobalo Tryphone hafla iliyofanyika kituoni hapo hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akiwakabidhi moja ya Mifuko ya Chandarua kwa watoto wa kituo cha Friends of Don Bosco klichopo Kimara jijini Dar es Salaam wakati benki hiyo ilipokabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5/- hafla iliyofanyika kituoni hapo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Christine Manyenye akikabidhi moja ya madumu ya mafuta ya kula kwa wanafunzi wa kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam wakati ilipokabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5/- hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akiwakabidhi moja ya Madaftari na Vitabu wanafunzi wa kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam wakati ilipokabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5/- hivi karibuni.
Baadhi ya watoto yatima wa Kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam wakicheza ngoma ya Mganda wakati wa hafla wa kukabidhiwa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5/- vilivyotolewa na Benki ya KCB Tanzania hivi karibuni.

Na Theeastaafrica Bloger

JAMII ya Kitanzania, imeaswa kuwaangalia kwa jicho la huruma watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalum ili kuwaweza kuishi vizuri na kujiona kuwa ni sehemu ya jamii pamoja na mapungufu waliyokuwa nayo.


Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto ya tima na wanoishi katika mazingira magumu cha Friends of Don Bosco iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Dk Edmund Mndolwa alisema makundi maalumu yanahitaji upendo na msaada wa wana jamii ili waweze kuishi vizuri.


Dk Mndolwa alisema kuwa, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa kuyasaidia makundi hayo na ndiyo maana kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii ime kuwa ikiyapatia misaada mbalimbali ya kijamii.


“Leo Benki ya KCB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali na vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni nne na nusu. Msaada huu siyo mkubwa sana lakini ni wazi kuwa utawasaidia watoto wanaolelewa katika kituo hiki. Makampuni mengine na watu binafsi wanapaswa kutambua kuwa hata kidogo walichonacho wakikitoa kinaweza kuleta tofauti,” alisema


Mwenyekiti huyo alisema kuwa msaada utitolewa na Benki ya KCB ni muendelezo misaada mbalimbali ambayo Benki hiyo inaitoa mwaka hadi mwaka na kuongeza kuwa kwa kipindi hiki cha Octoba hadi Desemba benki ya KCB imetenga shilingi milioni 180 kwa ajili ya kuisaidia jamii.

Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa kituo hicho Theobald Triphone alisema kuwa msaada uliotolewa na benki ya KCB umekuja wakati muafaka kutokana na kuwa kituo kinakabiliwa na matatizo mengi.

“Msaada huu kwetu ni mkubwa sana . Kituo kinakabiliwa na matatizo mengi na kibaya zaidi hatuna mfadhili wa kudumu jambo ambalo ni tatizo kubwa. Watoto hawa ambao baadhi ni yatima na wengine waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu wahitaji chakula,malazi, mavazi na elimu, tunawaomba wana jamii waiige benki ya KCB kwa kuwasaidia,” alisema


Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vitanda, magodoro, vyandarua, mashuka, madaftari, kalamu, unga, maharage, mchele sukari pamoja na mafuta ya kupikia.

No comments:

Post a Comment