Thursday, October 6, 2011

HUDUMA YA VING'AMUZI VYA STARTIMES YASITISHWA KWA MUDA BAADA YA BAADHI YA MITAMBO KUUNGUA NA MOTO!

Jengo la Huduma kwa wateja la Kampuni ya Star Media Group lililopo eneo la Televisheni ya Taifa TBC1 limenusurika kuungua baada ya kutokea mlipuko ulioanzia kwenye transfoma inayoingiza umeme kwenye jengo hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa moto huo ulianzia kwenye transfoma hiyo iliyokuwa kwenye uangalizi baada ya kubadilishwa baada ya iliyokuwa iktumika awali kulipuka Octoba 4 mwaka huu.


Akizungumzia tukio hilo Meneja wa Tanesco mkoa wa Kinondoni Mhandisi CHRISTOPHER MASASI amesema bado hawajabaini chanzo cha mlipuko huo ulioleta madhara kwa jenereta na moja ya chumba cha mitambo cha kampuni hiyo.
Kwa upande wake Afisa wa Kikosi cha Zimamoto cha Halmashauri yak Jiji la Dar es Salaam Sajenti YUSUFU MKALI amesema wamefanikiwa kudhibiti moto huo usilete madhara zaidi ingawa zoezi hilo lilichelewa kwa muda.
Hata hivyo kituo hiki kilitaka kupata ufafanuzi kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusiana na chanzo cha moto huo na kama kuna madhara yoyote kwa binadamu. Kamanda wa Polisi Mkoa maalum wa Kinondoni ACP CHARLES KENYELA anatoa ufafanuzi.


Kutokana na moto huo huduma zinazotolewa na Kampuni ya Star Media Group kupitia ving’amuzi vyake vya Star Times zimesitishwa. GLORY ZHANG ambaye ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo anatoa ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment