Wednesday, September 21, 2011

ZARINA MADABIDA ATAKA TAWLA WAMTETEE MKUU WA WILAYA YA IGUNGA KWA KUDHALILISHWA!

Chama cha Wanasheria Wanawake kimeombwa kuhakikisha kinamtetea Mkuu wa Wilaya ya Igunga kufuatia kitendo cha udhalilishaji alichofanyiwa na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Mbunge wa Viti Maalum kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Zarina Madabida amesema kitendo alichofanyiwa Mkuu huyo wa Wilaya ni kinadhalilisha haki na utu wa mtu hivyo hakina budi kupingwa kwa nguvu zote.

No comments:

Post a Comment