Monday, September 19, 2011

MALIPO DUNI YAHAMISHA ASILIMIA 81 YA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA NCHINI!

            Baadhi ya akina mama wakisubiri kupatiwa huduma ya afya katika moja ya Zahanati

Imeelezwa kuwa malipo duni pamoja na motisha hafifu kwa watumishi wa sekta ya Afya nchini, kumepelekea zaidi ya asilimia 81 ya wafanyakazi hao kuikimbia kazi hiyo na kuelekea kwenye fani nyingine ikiwa ni pamoja na kuhamia nje ya nchi.

Akizindua Ripoti kuhusiana na hali halisi ya wafanyakazi wa sekta ya afya nchini jijini Dar es Salaam, Meneja Mpango huduma za Afya ya Mama na Watoto, kutoka Shirika la Save the Children, DK. RACHEL MAKUNDE, amesema Tanzania ina wafanyakazi wa afya 35,000 tu katika maeneo ya kazi huku kukiwa na uhaba wa watumishi 88,000.


Amesema kufuatia hali hiyo, Tanzania ipo katika nafasi ya 30 ya nchi ambazo huduma zake za afya ni duni ambapo imedaiwa mtoto yupo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua.

No comments:

Post a Comment