Wednesday, September 21, 2011

SERIKALI YAKIRI WAJASIRIAMALI KUANZA KUBORESHA BIDHAA ZAO!

Serikali imekiri kuwepo kwa matokeo mazuri katika suala zima la kukuza ajira nchini baada ya wajasiriamali wengi kuanza kuboresha bidhaa na shughuli zao na hivyo kutoa mianya kwa ajira kupatikana kwa wingi.

Hayo yametihibitishwa na Naibu waziri wa kazi na ajira Dkt. MAKONGORO MAHANGA wakati akizindua mchakato wa maandalizi ya ushiriki wa wajasiriamali wa Tanzania kwenye maonesho ya kumi na mbili ya jumuiya ya afrika Mashariki ya nguvu kazi na jua kali yanayotarajiwa kufanyika nchini UGANDA Desemba mosi mpaka 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment