Wednesday, September 21, 2011

BALOZI WA RWANDA NCHINI FATMA NDAGIZA ATAKA WATANZANIA WADUMISHE UMOJA NA AMANI ILIYOPO NCHINI!

Watanzania wametakiwa kudumisha umoja na amani ya nchi iliyodumu kwa takribani miaka 50, jambo litakalochangia kasi ya kukua kwa uchumi endelevu utakaowezesha wananchi kujiletea maendeleo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Balozi wa Rwanda nchini BI FATMA NDAGIZA ametoa wito kwa Watanzania kuienzi amani iliyopo ili kutoa fursa kwa viongozi kuendelea kuongoza kwa kufuata misingi ya demokrasia.


Akitoa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Naibu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP,LOUISE CHAMBERLAIN amesema demokrasia haitokei tu, inabidi ilelewe, kukuzwa na kutetewa. Kauli mbiu ya siku ya amani mwaka huu ilikuwa ‘“ Amani na demokrasia, fanya sauti yako isikike”.

No comments:

Post a Comment