Monday, September 19, 2011

WAKAZI WA MKUZI MUHEZA TANGA WALALAMIKIA ENEO LAO KUKOSA MAJISAFI YA BOMBA!

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mkuzi Wilayani Muheza mkoani Tanga wamelalamikia kitendo cha eneo hilo kukosa maji safi na salama ya kunywa wakati kukiwa na mto Zigi unaopita kijijini hapo na maji yake kwenda kuvunwa kwa ajili ya wakazi wa jiji hilo.

Akizungumza na kituo hiki mmoja ya wakazi wa Kijiji hicho YOHANA VICENT amesema licha ya eneo hilo kupata maji kwa mgao, baadhi ya wafanyabiashara wanatumia fursa hiyo kwa kuwaletea maji kutoka jijini Tanga ambapo huwauzia ndoo moja kwa shilingi mia tano.


Kutokana na hilo mkazi huyo ameiomba serikali ya mkoa wa Tanga kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kuweka chujio litakalosambaza maji kulingana na mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment