Katibu Mkuu DAVID JAIRO akipokelewa kwa mbwembwe Wizarani hapo.
Hapa akiomba kabla ya kuanza kazi rasmi, hatimaye amesimamishwa kazi.
Kitendo cha serikali kumsimamisha kazi tena aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw DAVID JAIRO na kumwacha madarakani Katibu Mkuu Kiongozi Bw PHILEMON LUHANJO kimetajwa kama uchovu wa kufikiri unaofanywa na serikali katika kutoa maamuzi.
Akizungumzia malumbano yanayoendelea baina ya misingi miwili ya dola ambayo ni Serikali na Bunge Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw JAMES MBATIA amesema kwa kuwa bunge lilishabainisha tuhuma dhidi ya Bw JAIRO Katibu Mkuu Kiongozi LUHANJO alitakiwa kulishirikisha Jeshi la Polisi na TAKUKURU katika uchunguzi wake kabla ya kutoa uamuzi.
Kutokana na hilo MBATIA ameliomba Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuwawajibisha viongozi wote wanaokiuka taratibu ili kuondoa mianya ya ufisadi iliyopo kwenye baadhi ya Wizara nchini.
No comments:
Post a Comment