Shirika la Afya na Utafiti Afrika (AMREF) Tanzania limetoa wito kwa serikali kutenga rasilimali maalum zitakazosaidia kutekeleza miradi mbalimbali inayohusu sera na haki ya afya ya uzazi kwa vijana hususani kwenye mikoa ya Iringa na Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa AMREF nchini DK FESTUS ILAKO amesema bila serikali kulilinda kundi hilo taifa halitakuwa na maendeleo endelevu kwani takwimu zinaonesha kwamba theruthi moja ya idadi ya Watanzania ni vijana.
Nae Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw KAJUBI MKAJANGA ametoa wito kwa vijana nchini kupaza sauti zao katika kudai sera na haki za afya ya uzazi katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment