Thursday, August 25, 2011

WANASIASA WANACHANGIA VIFO VINAVYOTOKANA NA UZAZI KWA VIJANA KUONGEZEKA!

Kitendo cha Wanasiasa nchini kushindwa kuzungumzia afya ya uzazi kwa vijana kimechangia kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na ukosefu wa elimu na haki ya afya ya uzazi kwa vijana kuanzia umri wa miaka 10 hadi 24.

Akitoa mada kwenye semina elekezi kuhusiana na haki ya afya ya uzazi kwa vijana iliyoandaliwa na Shirika la Afya na Utafiti Afrika (AMREF) Tanzania, Muelimishaji LILIAN KALAGHE amesema kama wanasiasa hawatavunja ukimya ni wazi vijana vitendo vya ukatili na mimba zisizotarajiwa halitakoma.


Nae AGNESS KABIGI ambaye ni Meneja Mawasiliano na Utunishaji Mifuko wa AMREF Tanzania alitoa wito kwa jamii kutozikumbatia mila na desturi zinazowakandamiza vijana kushindwa kupata taarifa sahihi kuhusiana na haki ya afya ya uzazi.

No comments:

Post a Comment