Saturday, August 13, 2011

CHODAWU YAVUNJA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA!


Anna Titus na Esther Muze
Maelezo,Dar es Salaam
Baraza kuu maaluum la CHODAWU limevunja kamati ya utendaji ya Taifa iliyokuwepo na kutengua uteuzi wa aliyekuwa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu Bwana Kiwanga Towegale.

Taarifa iliyotumwa kwa Idara ya Habari (MAELEZO) iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza Kuu maalum Bwana Paul Msilu imesema licha ya kutengua nafasi ya Katibu Mkuu CHODAWU baraza hilo limeondoa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu aliyokuwa nayo Bwana Francis Maembe.


Aidha Baraza hilo limechagua Kamati mpya ya utendaji ya Taifa itakayosimamia shughuli za uendeshaji kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ambayo itaongozwa na Bwana Said Wamba.Taarifa hiyo imefafanua kuwa,Bwana Said Wamba ataiongoza Kamati mpya ya utendaji ya Taifa katika kipindi cha mpito cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mapema mwanzoni mwa mwezi Septemba 2011.


Pia Baraza Kuu limeomba wanachama na wadau wote kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo mpya katika kutekeleza jukumu la kuratibu shughuli zote za uchaguzi. Maamuzi ya Baraza hilo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam tarehe 3,Agosti 2008.

No comments:

Post a Comment