Friday, August 19, 2011

ANAYETUHUMIWA KUVAMIA KIWANJA CHA MJANE SAKUVEDA AKANUSHA SUALA HILO!

Askari Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ), Bw ALEX TIMOS BURA, anayetuhumiwa kuvamia kiwanja kilichopo Mbezi Sakuveda, Kata ya Kawe Jijini Dar es salaam, amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa anamiliki kiwanja hicho kihalali.

Akizungumza na kituo hiki Bwana BURA, amedai kusikitishwa na tuhuma hizo zilizotolewa na Mjane Bi KHADIJA MUSSA, Mkazi wa eneo hilo na kudai kuwa anamiliki kiwanja hicho kihalali baada ya kuuziwa na aliyekuwa Mume wa Mjane huyo ambaye kwa sasa ni marehemu.


Aidha kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya Wananchi pamoja na mjane huyo kuwa wanatishiwa kuuawa na Askari huyo Mstaafu wa JWTZ, kituo hiki kilifanya juhudi za kuonana na mwenyekiti wa eneo hilo ambaye hata hivyo hakuonyesha ushirikiano.

No comments:

Post a Comment