Friday, August 19, 2011

TAASISI YA USTAWI WA JAMII YAAJIRI WAHADHIRI WAPYA 18, CHUO KUFUNGULIWA JUMATATU!

Siku kadhaa baada ya Wahadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam kusitishiwa ajira zao kwa sababu ya kusababisha mgomo usio halali ili kuushinikiza uongozi kutekeleza madai yao mbalimbali ikiwemo kuwaongezea mishahara, uongozi wa chuo hicho kupitia Bodi ya Magavana umeajiri wahadhiri wapya 18 ili kufidia pengo hilo.

Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo Bw MWANDE MADIHI amethibitisha suala hilo na kuongeza kwamba wahadhiri hao wapya wataanza kazi rasmi baada ya chuo hicho kufunguliwa Agosti 22 mwaka huu.


Katika hatua nyingine uongozi huo pia umewaomba wanafunzi wa chuo hicho kutoa ushirikiano kwa wahadhiri hao wapya na kuwaahidi kutojirudia kwa mgogoro uliojitokeza ili kuleta maendeleo kwa taasisi na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment