Friday, August 19, 2011

TCU YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WALIODAHILIWA MWAKA WA MASOMO 2011/2012!

Tume ya Vyuo Vikuu nchini ( TCU), imetangaza majina ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2011/2012 katika vyuo vilivyoko chini ya tume hiyo.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. SIFUNI MCHOME, amesema wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka huo wa Masomo ni 31,093 kati ya wanafunzi 40,150 walioomba huku wengine 9,057 wakiwa wamekosa nafasi katika vyuo hivyo.


Prof. MCHOME, ameongeza kuwa wanafunzi 4,013 kati ya 9,057 waliokosa nafasi wamebainika kuwa na sifa lakini wamekosa nafasi katika vyuo hivyo kutokana na makosa mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa ujazaji wa fomu zao ambapo wameongezewa muda hadi Agosti 22 mwaka huu ili waweze kutuma maombi tena.

No comments:

Post a Comment