Serikali imekiri kwamba tatizo la ajira kwa vijana ni hatari kwa usalama wa Taifa kama halitapewa kipaumbele kinachostahili katika utatuzi wake.Kufuatia hali hiyo Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Naibu waziri wa Kazi na Ajira Dk. MAKONGORO MAHANGA ameliambia Bunge, kuwa Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini zikiwemo sekta binafsi ,vyama vya kiraia ,washirika wa maendeleo na jamii yote katika kukabilina na changamoto hiyo.
Dk. MAHANGA alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum CATHERINE MAGIGE (CCM ) ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani na kutoa ajira kwa vijana ambao ni takribani nusu ya watanzania wote.
No comments:
Post a Comment