Wednesday, July 6, 2011

VURUGU KATI YA MACHINGA NA POLISI JIJINI MWANZA LEO!

Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.

Wakati huo huo jijini mwanza kumezuka vurugu zilizopelekea watu wapatao 20 kutiwa nguvuni na jeshi la polisi kufuatia vurugu zilizozuka mapema hii leo.

Taarifa za awali zilisema kutoka jijini Mwanza kwamba kumezuka vurugu kubwa kati ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga na Polisi jijini humo baada ya wafanyabiashara hao kukaidi kuondoka eneo la msikiti mtaa wa Makoroboi kwa madai kwamba jeshi la Polisi linakiuka makubaliano waliojiwekea kati yao na Halmashauri ya jiji la Mwanza.

              Kamanda Sirro akiwaongoza wafanyabiashara wadogo kutawanyika.
Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
           Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.              Kuvunjwa vioo kwa jengo hili la msikiti wa hindu ni moja kati ya hasara zilizojitokeza.Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza haliiliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa..Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.
Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.

No comments:

Post a Comment