Thursday, July 14, 2011

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUWA WAVUMILIVU WAKATI SUALA LA MUUNGANO LIKIENDELEA KUJADILIWA!

                                                         Waziri mkuu MIZENGO PINDA
Serikali imewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati suala la muungano wa Tanganyika na Zanzibar likiendelea kujadiliwa kwa lengo la kuondoa kasoro zilizopo hivi sasa.

Rai hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri mkuu MIZENGO PINDA wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wabunge.


Waziri Mkuu PINDA amesema wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kuwa suala hilo bado linaendelea kujadiliwa hasa ikizingatiwa kwamba hivi sasa taifa linaingia katika mchakato mpya wa mabadiliko ya katiba.

                                                              MAUA ABEID DAFTARI
Mbunge wa Viti maalum kupitia Chama cha mapinduzi CCM MAUA ABEID DAFTARI ameitaka Serikali kuharakisha kuanza kutumika kwa Mkongo wa mawasiliano ambao utaunganisha mikoa yote nchini pamoja na nchi Jirani.
Mbunge huyo amebainisha hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Fedha katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.


Amesema sambamba na hatua hiyo pia Serikali inatakiwa ichukue hatua za haraka na Dharura za utoaji wa mafunzo ya kukabiliana na wizi kwa njia ya mtandao ambao unaweza kuwa ni tishio kwa mabenki mengi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment