Friday, November 4, 2011

BILL HYBELS KUTOA MAFUNZO YA UONGOZI UBUNGO PEAL NOVEMBA 7, 2011


Na Mdau wa Theeastafrica Blog,
Na Andrew Chale
RAIS wa shirika la Kimataifa linalotoa huduma za kiroho duniani la la Willow Creek Community Church, Mchungaji Bill Hybels ametua nchini kwa kutoa mafunzo maalumu juu ya uongozi kwa viongozi wakiwemo viongozi wa siasa,dini,seke mbalimbali pamoja na wafanyabiashara katika ukumbi wa Ubungo Peal, utakao fanyika Novemba 7,2011,Jumatatu.

Kiongozi huyo Raia wa Marekani alitua mapema mchana wa leo jijini Dar es Salaam na hiyo Novemba 7, anatarajia kuongoza mkutano mkubwa juu mafunzo ya uongozi kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wanasiasa,wafanyabiashara,mashehe,maaskofu na wa sekta nyingine hapa nchini ambapo Makamu wa Rais Dk. Mohamed Garib Bilal utakaofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Peal.


Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege muda mfupi wakati wa kuwasili kwa kiongozi huyo, mratibu wa The Global Leadership Summit Tanzania ambaye pia ni mkurugenzi wa Shirika la huduma ya Sauti ya Matumaini (VHM) Peter Mitimingi alisema kua kiongozi huyo mashuhuri amebobea katika mafunzo ya uongozi na ujio wake utakua na faida mbalimbali kwa watakaopata mafunzo yake.
“Mafunzo yatakayotolewa na Bill Hybels ni ya hali ya juu hasa kutokana na kubobea kwenye ufundishaji wa uongozi na kupata heshima duniani kote” alisema, Mitimingi. Pia alisema kua Tanzania wataelewa nini maana kati ya uongozi na utawala..ilikutofautisha vitu hivi viwili hivyo watakapata mafunzo haya watapiga hatua kwenye uongozi wao, alimalizia,Mitimingi.


Kwa upande wake, Kiongozi huyo alipowasilini uwanjani hapo na kupokelewa na wenyeji wake kwa nderemo, alipongeza mapokezi hayo ya aina yake na kuwaidi kufanya kitu kikubwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment