Monday, July 25, 2011

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA NALIENDELE MTWARA!

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais JAKAYA KIKWETE ameongoza mamia ya Watanzania, viongozi mbalimbali na mabalozi wanaowakilisha nchi zao kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa kwenye eneo la Makaburi ya mashujaa Naliendele mkoani Mtwara.

Kabla ya kuweka mkuki na ngao za asili kwenye mnara wa kumbukumbu wa mashujaa, Rais KIKWETE alipokea heshima maalum kutoka kwa kikosi maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na baadae kutembelea baadhi ya makaburi na mabanda ya maonesho yaliyopo kwenye viwanja hivyo.

Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo yak siku ya kumbukumbu ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK ALLI MOHAMED SHEIN, Makamu wa Rais DK GHALIB MOHAMED BILAL, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali DAVIS MWAMNYANGE.

No comments:

Post a Comment