Sunday, July 24, 2011

REDDS MISS ILALA KUONYESHANA VIPAJI JUMATATU SAVANNAH LOUNGE.

Warembo wa Redds Miss Ilala 2011 waliokuwa kwenye ziara ya Kimafunzo na Utalii katika Majiji ya Nairobi na Arusha wanarejea leo na watapanda jukwaani kupambana katika shindano la vipaji siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Savannah Lounge ulioko Pugu Rd - jengo jipya la Quality Centre.

Shindano la vipaji ambalo ni fungua pazia la shindano kubwa la Miss Ilala, linafanyika huku majigambo na kutambiana kukiwa kumeshika kasi miongoni mwa Warembo. Warembo wataonyesha vipaji vyao kwenye kuimba, kucheza muziki, kucheza ngoma za kiasili, kuchora na kuigiza.
Warembo watano watakaofanya vizuri zaidi watachaguliwa na Majaji kufanya maonyesho yao kwenye fainali zitakazofanyika siku ya Ijumaa tarehe 29 Julai, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Shindano la Vipaji la Redds Miss Ilala lilikuwa limepangwa kuhudhuriwa na wageni maalum tu, lakini kutokana na maombi ya watu mbali mbali wakiwemo warembo tumelazimika kufungua milango kwa watu wote ili kila mwenye hamu ya kuona aweze kuingia kuingia savannah Lounge na kuwaona warembo katika full vipaji. Wageni ambao watahudhuria tamasha hili bila kuwa na mwaliko, watalazimika kulipa kiingilio mlangoni cha Shs, 10,000/-
Safari ya Nairobi na Arusha imewaongezea upeo na kujiamini maana warembo wengi walikuwa hawajawahi kusafiri hata nje ya Dar es salaam. Sasa wana ufahamu wa kutosha baada ya kukutana ana watu mbali mbali walipokuwa safarini na kujifunza kuhusu urembo.
Onyesho la kufunga mashindano ya Kanda kuelekea shindano la Vodacom Miss Tanzania litafanyika siku ya vunja jungu, ijumaa tarehe 29 julai 2011. Hili litakuwa shindano la kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania na linategemewa kuwa ndilo shindano litakalo mtoa mwali wa Miss Tanzania mwaka huu.

Shindano hili limedhaminiwa na Redds Original, Vodacom, Paradise city Hotel, Paris Pub ya Tabata, Habari leo, TV Sibuka, Syscorp Group, Michuzi Blogspot, B2C, Papazi entertainment, Jamboleo, Channel ten, Clouds FM na Clouds TV, Aurora na Sofia Production na litashirikisha Warembo kumi na saba ambao ni Maria John Mrema, Jenifer Kakolaki, Priscilla Mschema, Nasra Salim, Diana John, Faizal Ally, Maryvine Nkezia, Godliver Mashamba, Edna Mnada, Salha Israel, Augostina Mshanga, Lilian Paul, Mariam Manyanya, Williet Rwechungura, Liliam William na Alexia William.

No comments:

Post a Comment