Sunday, July 10, 2011

MUFTI WA OMANI, SHEIKH AHAMED BIN HAMAD ALKHARIL AOMBA WATANZANIA WADUMISHE AMANI ILIYOPO!

Mufti Mkuu wa nchi ya OMAN, Sheikh AHAMED BIN HAMAD ALKHARIL amewataka Watanzania kudumisha amani iliyopo nchini sanjari na kuheshimu utawala uliopo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Sheikh AHAMED ambae yupo nchini kwa ziara ya siku tano, amesema lengo la ziara hiyo ni kuwatembelea baadhi ya ndugu waliopo nchini ikiwa ni pamoja na kuenzi udugu ulipo baina yake na Watanzania.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ALHADI MUSSA SALUM, amesema anatarajia Mafanikio makubwa kutokana na ziara hiyo huku akitoa wito kwa Waislamu kote nchini kutumia nafasi hiyo kujifunza kupitia mihadhara mbalimbali itakayofanywa na mufuti huyo.

No comments:

Post a Comment