Wednesday, July 6, 2011

MBUNGE WA KISARAWE ATAKA MAFUVU YA WATU WALIOUAWA NA ASKARI WANYAMA PORI YARUDISHWE!

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imegwaya kutoa majibu sahihi kuhusiana na mauaji ya wakazi wawili wa tarafa ya Chole Wilayani Kisarawe yaliyofanywa na askari wa Idara ya Wanyamapori kwa madai ya kuingia bila kibali kwenye pori la akiba la Selous.


Mbunge wa Kisarawe (CCM) SELEMANI JAFO aliiuliza serikali uhalali wa askari hao kuua raia wasiokuwa na hatia na kuwachoma moto ambapo amehoji lini mafuvu ya vichwa yaliyochukuliwa kwa ajili ya uchunguzi yatarudishwa kijijini hapo kwa ajili ya mazishi.


Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii EZEKIEL MAIGE amesema kwa kuwa wizara yake ndiyo watuhumiwa wanaliacha suala hilo jeshi la Polisi nchini kwa ajili ya ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment