Wednesday, July 27, 2011

HII NDIO SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU DANNY MWAKITELEKO (TUTAKUKUMBUKA DAIMA)!

Wahariri wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mhariri mwenzao, marehemu Mwakiteleko wakipeleka kwenye nyumba yake ya milele katika Kijiji cha Ndala.
Baadhi ya wahariri na waombolezaji wengine wakilia kwa uchungu baada ya mwili wa aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006), marehemu Danny Mwakiteleko kuwekwa kwenye nyumba yake ya milele, katika Kijiji cha Ndala, Mwakaleli, Tukuyu, mkoani, Mbeya jana.
     Mjane wa marehemu, Mwakiteleko, Winnie akiweka shada la maua katika kaburi la mumewe.

Mwili wa mpendwa Danny Mwakiteleko ukipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kijijini kwao Ndala.
Watoto wa marehemu, Mwakiteleko, Vanesa (kulia) na Caroline wakiwa na huzuni wakati wa mazishi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari , wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa boss wao. PICHA ZOTE KWA HISANI YA FULL SHANGWE BLOGSPOT.

No comments:

Post a Comment