Tuesday, July 12, 2011

DK KILAHAMA AWATAKA WATAFITI KUTATHIMINI KWA AJILI YA MASLAHI YA WATANZANIA!

DK Felician Kilahama akiwa na Waziri Ezekiel Maige.
                                                                  Misitu ya Asili
Imeelezwa kwamba licha ya kuanzishwa kwa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Taasisi ya Utathimini Rasilimali za Taifa IRA kuhusiana na Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi kuna wasi wasi kwamba lengo huenda lisifikiwe iwapo elimu ya utafiti huo haitaenezwa kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dakta FELICIAN KILAHAMA amesema watafiti wengi wamekuwa wakipandishwa vyeo kwa kufanya tafiti na kuchapisha kwenye makabrasha badala ya kuweka uzalendo mbele kwa kufanya tathimini zinazoweza kusaidia kubadilisha maisha ya Mtanzania.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Taasisi ya Utathimini Rasilimali za Taifa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam IRA HILDA KIWASILE ametoa wito kwa vyuo vya taaluma kuacha mtindo wa kufundisha kwa nadharia ili tafiti mbalimbali zinazofanywa ziboreshe mikakati ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment