Thursday, June 16, 2011

UNICEF LATOA RIPOTI YAKE JUU YA HALI YA WATOTO BARANI AFRIKA!

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika kuwahudumia watoto duniani UNICEF limetoa ripoti yake juu ya hali ya watoto katika bara la Afrika huku likizitaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwalinda watoto.

Shirika la Unicef limearifu kwamba barani Afrika kila siku watoto wanakabiliwa na ghasia,kutumiwa vibaya na kubakwa.
Siku ya mtoto wa Kiafrika inayoadhimishwa kila mwaka ilianzishwa na shirika hilo la UNICEF miaka 21 iliyopita.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inawataka watu wote katika jamii kushirikiana kuchukua hatua za dharura kuwasaidia watoto wa mitaani.
Aidha Unicef limezitaka serikali kutatua chanzo kinachosababisha utengano wa familia hali ambayo baadae husababisha watoto kujikuta mitaani wakitafuta msaada.

No comments:

Post a Comment