Thursday, June 23, 2011

DK BILAL AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU TATU YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE

Mmoja kati ya washiriki ambaye pia ni mjasiliamali wa katika Mafunzo hayo, Alya Riyami, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya ufunguzi huo.

Wafanyakazi wa Benki ya NBC, Mshauri wa Mawasiliano katika benki hiyo, Robi Matiko (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula, wakiwa ndani ya ukumbi huo wakati wa ufunguzi wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiliamali, yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko huo. Mama Anna Mkapa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment