Tuesday, June 7, 2011

DHAMANA YA MBOWE ILIFUNGULIWA TENA HIVI JIJINI ARUSHA!

Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM limewaonya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kuacha mara moja vitendo vya kuwatumia vijana kama chambo katika uchochezi utakaosababisha luvunja amani nchini.

Kauli hiyo inafuatia baada ya hapo jana viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kudaiwa kuwashinikiza vijana kuingia mitaani wakiwa wamevaa fulana na mabango yenye ujumbe unaochochea nchi kuingia katika machafuko ya umwagaji damu.

Katika hatua nyingine Kamanda KOVA alipotakiwa kufafanua kwa undani kwa nini Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bwana FREEMAN MBOWE kusafirishwa na na ndege ya Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kutoka DSM mpaka mkoani ARUSHA . . . .alijibu kama ifuatavyo.


Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti huyo hapo jana ameachiwa baada ya hati yake ya dhamana iliyokuwa imefutwa na mahakama baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamani kufunguliwa upya.


Wakati huohuo Mwenyekiti huyo amekili kusafirishwa na Na Ndege ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ kutoka Jijini DSM mpaka Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment