Friday, May 13, 2011

SERIKALI YAKIRI KUKOSEKANA KWA UPENDO KUNACHANGIA ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI!

                                                                   SOPHIA SIMBA
                                Moja ya mtoto wa mitaani akiwa amejipumzisha mtaani!
Serikali imekiri kwamba kukosekana kwa upendo na mshikamano kwenye ngazi ya familia huchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la watoto wa mitaani ambao wanakosa haki zao za msingi ikiwemo kuendelezwa katika masuala yanayowahusu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusiana na maadhimisho ya siku ya familia Duniani yatakayofanyika Mei 15 mwaka huu, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi SOPHIA SIMBA amesema ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ni tatizo linalozikabili familia nyingi nchini na jitihada zinahitajika ili kumaliza vitendo hivyo katika jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya familia duniani ni kupambana na umasikini katika familia ni jukumu la kila mmoja.

No comments:

Post a Comment