Tuesday, May 17, 2011

MBUNGE LUCY MAYENGA AKABIDHI VYEREHENI VYA MILIONI 2/- KWA UWT SHINYANGA!

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga, LUCY MAYENGA, leo amekabidhi vyerehani vyenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa UWT, kata zote za manispaa ya Shinyanga, pamoja na fedha taslimu kwa waendesha pikipiki wa manispaa hiyo, lengo likiwa ni kuwasaidia kwa pamoja kuanzisha vikundi vya saccos.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama Bi Juliana Lucasambaye ni mwenyekiti wa UWT kata ya Kivumbi amesema wanamshukuru mbunge huyo na kuahidi kuvitumia kama njia ya kujipatia kipato.

No comments:

Post a Comment