1. UTANGULIZI
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency) –TFS- umeanzishwa kwa kuzingatia Sheria ya Wakala wa Serikali Namba 30 ya 1997 iliyorejewa 2009). TFS ilianza kazi rasmi Julai 1, 2011 ikiwa na lengo la kutekeleza majukumu ya kiutendaji ya uhifadhi na usimamizi wa rasimali za misitu na nyuki kwa ufanisi na tija zaidi.
Wakala unatakiwa kuendesha shughuli za uhifadhi na usimamizi wa rasimali za misitu na nyuki kwa kujitegemea kwa asilimia 100 pamoja na kuchangia fedha katika mfuko mkuu wa Serikali yaani Hazina. Ili kufikia azma hii Wakala unajizatiti katika kudhiti biashara haramu ya mazao ya misitu inayofanywa kinyume cha sheria na kuboresha ukusanyaji wa maduhuli, kubaini mianya iliyopo ya ukwepaji kulipa ushuru wa mazao ya misitu na kutafuta mikakati ya kuidhibiti.
2. HATUA TULIZOCHUKUA
Wakala umefanya ukaguzi maalum wa namna biashara ya mazao ya misitu na ukusanyaji maduhuli inavyosimamiwa katika maeneo mbalimbali ili kubaini na kujionea hali halisi katika kudhibiti biashara ya mazao ya misitu na kukusanya maduhuli kwa nchi nzima kuanzia tarehe 7/05 – 21/05/2012.
Katika ukaguzi huo makundi 11 yalifanya kazi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuboresha ukusanyaji maduhuli, kuimarisha makusanyo na kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu nchini. Ukaguzi na uhakiki wa nyaraka ulifanyika katika Ofisi za Maafisa Misitu Wilaya, Maafisa wa Vituo vya Ukaguzi, maeneo ya uvunaji na kwa wafanyabiashara ili kuangalia kama taratibu, kanuni na sheria dhidi ya kumiliki na kusafirisha mazao ya misitu zinazingatiwa. Kazi hii ilifanyika usiku na mchana.
3. CHANGAMOTO
3.1 MAMBO TULIYOJIFUNZA
Tathmini ya zoezi hili imefanyika na kutuonyesha changamoto zinazotukabili katika maeneo yafuatayo:-
(i) Usimamizi wa rasilimali za misitu
(ii) Mfumo wa Utendaji
(iii) Watumishi na Vitendea Kazi mfano Usafiri na Nyaraka.
No comments:
Post a Comment