Friday, May 4, 2012

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 28 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mkutano Mkuu  wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulioanza leo Mei 4 2012 katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kitabu cha muongozo wa maazimio ya kazi za Tawala za mitaa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (TAMISEMI) Agrey Mwanri, mara baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) alioanza leo katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter BRANDES, (kulia) ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mshauri wa TFDA, Octavian Soli, wakati alipokuwa akitembelea na kuzindua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo Mei 4, 2012 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meneja Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Iman Kajula, wakati  wakati alipokuwa akitembelea na kuzindua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo Mei 4, 2012 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la Viwanja vya Hoteli ya Kunduchi Beach, baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo Mei 4, 2012 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

 
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kuhusu mashine za kufyatulia matofali ya gharama nafuu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Rubana Construction, Ibrahim Sherally, wakati alipokuwa akitembelea na kuzindua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ulianza leo Mei 4, 2012 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment