Wednesday, April 4, 2012

CCM NA HARAKATI ZA UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI.

Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni uliofanywa na wabunge kuwapata wagombea wa ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, Abdulrahman Kianana akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, jana.

 Katibu wa Wabunge wa CCM, akimkaribisha Mwenyekiti wa wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pindakusimamia uchaguzi wa wagombea wa Ubunge wa Afrika Mashariki. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo.



 Wagombea wa katika kura za maoni ubunge wa Afrika Mashariki wakinyoosha mikono kuunga mkonbo hoja wakati wa uchaguzi huo.



 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kukanusha kuhusika na kashfa ya mradi wa machinjio ya kisasa jijini Dar es Salaam, Kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila siku.


 Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akifafanua jambo katika mkutano huo na Waandishi wa habari.



 Wagombea wateule waliopita kwenye  kura za maoni wa ubunge wa Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Benki ya KCB Dk. Edmund Mndolwa na Mbunge aliyemaliza kipindi kimoja cha ubunge wa bunge hilo, Dk. Said Gharib Bilal wakijadili jambo, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam. Wateule wote wa kura za maoni katika uchaguzi wa kuwapata wagombea hao uliofanyika jana, waliitwa kwenye Ofisi hiyo ya CCM kwa hatua zaidi

No comments:

Post a Comment